Familia haitaki kufanya hivyo, Gerrie Nel alisema.Walisema tuzungumze na tuwache kesi hii, lakini hakuna kiwango cha fedha kilichotajwa ,aliongezea.
Bwana Nel anajulikana kwa jina la utani kama ''the Pitbull''. Alifanikiwa kumshtaki mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius kwa mauaji.
Wakati huohuo katika mahojiano marefu ya simu na bi Gabriella Engels ambaye amemtuhumu bi Grace Mugabe kwa kumpiga, Mwandishi wa BBC Pumza Fihlani alitulia na kuonekana kuwa mtu aliyekuwa na wasiwasi mwingi mara kwa mara.
Akielezea tukio hilo bi Engels mwenye umri wa miaka 20 alisema kuwa yeye na watu wengine wanne, wawili wakiwa wana wa kiume wa rais Mugabe na bi Grace Mugabe walikuwa wakinywa vinywaji siku ya Jumapili usiku katika chumba kimoja cha hoteli mjini Sandton, makaazi ya kifahari yaliopo Johannesburg.
Baadaye alienda katika chumba chengine na bi Mugabe akamfuata akiwatafuta wanawe.
Bi Mugabe alikuwa ameshikilia waya wa umeme mkononi mwake....alinizuia na kuanza kunipiga .
Nilijiangusha chini na kuanza kubingirika ili kukwepa kichapo hicho, na ni hapo aliponipiga na waya hiyo. Na nakumbuka nikiwa katika sakafu huku nikiwa nimejaa damu usoni na shingoni, bi Engels alidai.
Nilikuwa nikifikiria nitoke katika chumba hicho kabla ya mwanamke huyu kuniuwa.
Watu waliokuwa katika chumba hicho ni walinzi wake na walikuwa wamesimama nyuma yake huku akitupiga.
Tulimsihi kuwacha kufanya hivyo ,lakini hakutaka kusikia aliendelea kutupiga...alitupiga akiwa na chuki nyingi .
Hadi leo marafiki zangu sielewi kwa nini mwanamke huyu alitushambulia vile bila ya sababu yoyote, Engels aliongezea.
kabla nitambue alikuwa bi Mugabe, nilijua nilifaa kumshtaki kwa kunishambulia kwa kuwa nilijeruhiwa vibaya
Sikujua yeye ni nani. na nilipojua yeye ni nani, sikutaka kumshtaki .. lakini mamangu akanisukuma kuwasilisha mashtaka hayo mahakamani, kwa sababu aliniambia: Kile mwanamke huyu alichotenda sio sawa.
Hatuwezi kuruhusu kukwepa kitendo alichofanya, alisema bi Engels.
Mwanamke huyo wa miaka 20 alisema: Ningefurahia sana iwapo angepelekwa jela.. hilo ndio lengo langu kwa sasa.
Bi Mugabe hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
No comments:
Post a Comment