Sembi yupo katika kituo hicho kinachomilikiwa na mmiliki Super Sports, Farouk Khan amedai kuwa amekuwa na malengo ya kucheza barani Ulaya ndiyo maana imekuwa rahisi kwake kukataa ofa hiyo.
“Siyo Orlando pekee bali hata Santos na yenyewe ilikuwa inahitaji kunitumia kwa msimu huu mpya, lakini msimamo wangu ni kucheza Ulaya.
“Ni kisema nisaini mkataba itakuwa kama najifunga, mazungumzo yanaendelea baina wakala wangu akishirikiana na kituo changu ili nikacheze Ureno.
“Mungu akipenda naweza kuanza kuichezea Vitoria SC na kama kutakuwa na mabadiliko nitayaweza wazi” alisema Sembi.
Mwananchi:
No comments:
Post a Comment