Kwa mujibu wa habari,mwanajeshi mmoja amefariki baada ya mlipuko huo Cheorwon huku wengine sita wakiwa wamejeruhiwa.
Ripoti zinaonyesha kuwa mwanajeshi aliyepoteza maisha alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Seongnam katika jimbo la Gyeonggi.
Uchunguzi zaidi wa ni nini hasa kilichosababisha mlipuko huo katika mpaka unaolindwa na maelfu ya wanajeshi kutoka Korea Kusini na Kaskazini unaendelea.
Hata hivyo Pyongyang inaamini kuwa mashambulizi kama hayo ni dalili kuwa kulikuwa na njama ya uvamizi nchini humo.
No comments:
Post a Comment