Nyumba ya wageni yateketea kwa moto - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, August 24

Nyumba ya wageni yateketea kwa moto


Jengo ambalo limewaka moto.

Moto umelipuka katika nyumba ya kufikia wageni iliyopo Manzese Tip Top Jijini Dar es Salaam jirani na hoteli ya Iranda

Moto huo umesababisha nyumba zote za jirani kuhamisha vitu vyao kwa kuhofia nyumba zao kushika moto nazo pia huku wageni wageni waliyofikia katika nyumba hizo kukumbwa na taharuki ya kukimbia katika hoteli hiyo.

Moto huo ambao umeanza majira ya saa 1:30 asubuhi mpaka sasa chanzo chake hakijabainika kuwa ni nini, ingawa magari ya kuzima moto yameweza kufika kwenye eneo la tukio wakati moto huo ukiwa umekwisha kolea kwa kiasi kikubwa na kupelekea kuteketeza nyumba hiyo japo baadhi ta wataalum wameweza kufanikiwa kudhibiti usiweze kuenea katika majengo mengine yanayokaribiana nayo.

Taarifa kamili za tukio hili zitakujia hivi punde

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here