Wazimbabwe walivyozibeba Simba na Yanga kwenye Ngao ya Jamii - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, August 24

Wazimbabwe walivyozibeba Simba na Yanga kwenye Ngao ya Jamii


Kaama ulikuwa hujashtukia basi mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Yanga iliongozwa na manahodha wa kigeni wote wakiwa wanatoka Zimbabwe.

Thabani Kamusoko ni nahodha msaidizi wa Yanga, alivaa kitambaa cha unahodha kwa sababu nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub ‘Cannavaro’ hakuwa sehemu ya mchezo wa Ngao ya Jamii kwa sababu hakuwepo hata kwenye benchi.

Kwa upande wa Simba Method Mwanjale ndio nahodha mpya aliyepewa jukumu la kuiongoza klabu hiyo akichukua kitambaa kutoka kwa mzawa Jonas Mkude. Mwanjale pia ni raia wa Zimbabwe hivyo mechi ya Ngao ya Jamii ilikuwa chini ya manahodha wakigeni wanaotoka taifa moja.

Kama unakumbuka vizuri manahodha hawa walipiga penati kwenye mchezo huo baada ya timu zote kushindwa kufungana katika dakika 90 na kulazimika mshindi kupatikana kwa matuta. Wote walifunga penati zao, Mwanjale alipiga penati ya kwanza kwa Simba huku Kamusoko akifunga penati ya pili kwa Yanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here