Hayo yameibuka ikiwa imebakia siku moja kuelekea katika mechi ya watani wa jadi inayotarajiwa kupigwa siku ya Jumatano (kesho), ambapo kipindi chote baadhi ya wafanyabiashara huwa wanajipatia kipato chao kwa kuuza jezi za Yanga pamoja na vifaa vingine kwa wachezaji ambao wana lengo la kuingia ndani ya uwanja kutazama mechi.
"Klabu inatoa tahadhari (onyo) kwa watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine watashiriki kuuza vifaa au jezi zenye nembo ya Yanga SC kuanzia leo, watakamatwa na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao", alisema Dismas katika taarifa yake aliyoitoa.
Pamoja na hayo, Dismas aliendelea kwa kusema "kikosi maalum kimeandaliwa kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa jambo hili, na wahujumu wote watakamatwa".
Kwa upande mwingine, klabu ya Yanga kesho itashuka dimbani kuminyana na Simba huku ikiwakosa wachezaji wake watatu akiwepo mshambuliaji mwenye uraia wa Zambia Obrey Chirwa , Benno Kakolanya na Mwasiuya kutokana na kuwa majeruhi.
No comments:
Post a Comment