Breaking News: Lissu adaiwa kukamatwa - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, August 22

Breaking News: Lissu adaiwa kukamatwa


Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu  amedaiwa kukamatwa leo Jumatatu mchana akitokea  Mahakama ya Kisutu.

Mwanasheria  huyo alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi  lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere mahakamani hapo.

Akielezea ilivyokuwa Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likazuiwa  na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police.

Wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Police.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here