MFUMKO wa bei wa bidhaa mbalimbali umepanda kwa asilimia 1.4, kutokea 4.1 mwezi Julai mpaka 5.5 mwezi Agosti mwaka huu.
Kupanda kwa mfumko kunatajwa kuwa ni kutokana na bidhaa nyingi zinazotumika sasa zinaagizwa kutoka nje ya nchi sambamba na ongezeko la bei katika soko la dunia. Akitoa taarifa ya mfumko huo Afisa Mtakwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali hapa Zanzibar, Salma Saleh Ali amesema kuwa bei za bidhaa zimeongezeka kwa asilimia 1.4.
Alisema kuwa katika mwezi wa Agosti 2017, bidhaa za chakula na zisizo za chakula zimepanda kwa asilimi 6.1 ikilinganishwa na mwezi wa Julai 2017, ambapo ilikuwa ni asilimia 2.7.
Hata hivyo aliongeza kuwa kwa ujumla mfumko wa bei kwa mwaka kutoka Agosti ya mwaka 2016 umepanda hadi kufikia 105.2 kutoka 99.6 ya Agosti mwaka 2017. Pia alieleza kuwa mchele wa Mapembe umefikia asilimia 5.1, wakati mchele wa Mbeya upo asilimia 3.4, Jasmini asilimia 3.0, Basmati asilimia 1.9, Unga wa Mahindi asilimia 12.4, ndizi ya Mtwike asilimia 2.5 na ndizi ya mkono mmoja (Tembo) ni asilimia 3.2.
Sukari katika mwezi huu imepanda kwa asilimia 10.2 na Mafuta ya Taa 1.7, Petroli 1.5. Mhadhiri wa Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Dkt. Suleiman Simai Msaraka amesema kuwa pamoja na kupanda kwa mfumko huo wa bei, hali haitishi kwa sababu mfumko huo umepanda duniani kote.
Nae Mkuu wa Idara ya Kiuchumi za Takwimu Abdul Ramadhan alisema kuwa ili hali ya mfumko wa bei isijitokeze tena ni lazima watu wajenge tabia ya kutumia vyakula zaidi wanavyozalisha wenyewe pamoja na kurejeshwa utaratibu wa kuweka akiba katika maghala yao ya chakula ili viweze kutumika endapo kutakuwa na upungufu wa chakula.

No comments:
Post a Comment