Israel yashambulia kiwanda cha silaha Syria - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, September 7

Israel yashambulia kiwanda cha silaha Syria


Syria inasema kuwa ndege za jeshi la Israeli zimeshambulia kituo cha kijeshi magharibi mwa nchi huku ripoti zikiseka kuwa kiwanda cha silaha za kemikali zilishambuliwa.

Taarifa za jeshi zilisema kuwa makombora yaliyofyatuliwa kutoka anga ya Lebanon yalilenga kiwanda hicho kilicho karibu na Masyaf na kuwaua wanajeshi wawili.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa kiwanda ya kutengeneza silaha za kemikali kilishambuliwa.


Kisa hicho kinatokea siku moja baada wachunguzi wa Umoja wa Mataifa kusema kuwa serikali ya Syria ilihusika na shambulizi la silaha za kemikali katika mji unaoshilkiliwa na waasi mwezi Aprili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here