Umoja wa mataifa kwa upande wake umevitaka vyama vya siasa Kenya kuheshimu maamuzi ya mahakama na kujipanga kurudia uchaguzi huo kama ilivyoamuriwa.
Kenya ni nchi ya kwanza barani Afrika kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais ambapo uamuzi huo ulitolewa na Mahakama ya Juu nchini humo ambayo ilitoa uamuzi wa kihistoria wa kufuta matokeo ya uchaguzi na imeahidi kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu sababu zilizopelekea kutolewa uamuzi huo ndani ya siku 21.
Mahakama hiyo ya juu nchini humo inayoundwa na majaji saba ambao hukumu yao ni ya mwisho na isiyopingwa, iliundwa na katiba mpya ya mwaka 2010.
Kwa upande wa chama cha upinzani kilichofungua mashtaka hayo kimeonesha wasiwasi wake juu ya watendaji wa tume ya uchaguzi nchini humo IEBC na kutaka kufanyika kwa mabadiliko.
Uchaguzi mpya nchini Kenya unatarajiwa kufnayika ndani ya siku sitini tangu kufutwa kwa uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment