Bunge linasubiriwa kufunguliwa nchini Kenya leo ambapo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutoa hotuba.
Hata hivyo wabunge wa upinzani wamesema kuwa watasusia sherehe hiyo ya kufunguliwa kwa bunge, wakati kuna malumbano kuhusu marudio ya uchaguzi wa urais.
Hata hivyo hiyo jana Rais Kenyatta alisema kuwa shughuli za bunge zitaendelea kama kawaisa bila ya kewepo wabunge wa upinzani.
Bunge linafunguliwa huku wakenya wakijiandaa tena kupiga kura tarehe 17 mwezi Oktoba.
Mahakama ya juu zaidi nchini Kenya iliamrisha uchaguzi wa urais kurudiwa kutoka na hitilafu zilizotokea kwenye uchaguzi mkun uliofanyika tarehe 8 mwezi Agosti.
No comments:
Post a Comment