CCIB FM+, cha nchini Burundi mapema mwezi huu kilitoa taarifa za kukosoa mwenendo wa serikali baada ya mauaji ya warundi 36 katika maandamano ya sept 15 nchini Drc ambayo pia askari mmoja wa Drc aliuawa.
Mkurugenzi na muhariri Eddy Claude Nininahazwe aliiambia AFP kuwa kituo kimezuiwa kwa kutangaza ukimya wa serikali baada ya mauaji ya warundi.
Katika taarifa ya serikali baraza la habari lilidai kituo hiko kimefanya ukiukwaji wa maadili ya taaluma ya habari na sheria zinazosimamia vyombo vya habari na kukiamuru kuzima mitambo yake kwa miezi mitatu kuanzia jumatatu.
Nininahazwe amelaani hatua hiyo akijitetea kituo chake hakikuvunja sheria yoyote.
No comments:
Post a Comment