MKUTANO WA PAN AFRIKA UWE NA TIJA KWA VIJANA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, November 23

MKUTANO WA PAN AFRIKA UWE NA TIJA KWA VIJANA

Vijana ni tegemeo kubwa katika bara la Afrika na hususan katika ujenzi wa Taifa huku takwimu katika mataifa mbalimbali zikionesha kuwa idadi kubwa ya wananchi wao ni vijana licha ya wingi wao lakini bado vijana wanakosa fursa za uongozi na kulilia suala la ajira jambo ambalo limekuwa tatizo sugu linalopelekea vijana wengi kujiunga na makundi mbalimbali yenye uvunjifu wa amani na kutumiwa katika harakati za uvujifu wa amani.suali ibuka ni je nini kitawunganisha vijana wa kiafrika ambao ndio taifa la kesho?

viongozi waliohudhuria mkutano wa pan Africa 2017
Nadhani mutakubaliana na mimi kuwa sehemu yoyote panapokosekana amani pia maendeleo hukosekana na ili kuwe na amani lazima watu waungane pamoja ili kujenga mawazo na mitazamo chanya itakayopelekea kuimarika kwa amani na kuinua maendeleo ya bara la Afrika.
Tanzania imekua nchi ya kwanza Afrika mashariki kuandaa mkutano mkubwa wa panAfrica chini ya asasi ya vijana wa umoja wa mataifa almaarufu  Yuna Tanzania  pamoja na tuzo maarufu za Pan Africa Humaniterian awards. Huku kauli mbiu ya mwaka huu 2017 ikiwa ni "Amani inawezekana"


Kulingana na Arafat Bakiri makamo mwenyekiti asasi ya vijana wa umoja wa mataifakatika mahojiano na mwandishi wetu wakati wa mkutano huo alisema kuwa lengo la mkutano huo ambao ulifanyioka jijini Dar es salaam mapema wiki hii ulilenga zaidi vijana ili kuwajenga kiungozi na kudumisha amani katika bara la Afrika "Lengo la mkutano huu mkubwa wa leo tumewazingatia zaidi vijana ili kuwajenga kiungozi na jinsi kuwa na Amani katika nchi zetu za Afrika" alisema Bakiri.
Arafat Bakir naibu mwenyekiti asasi ya vijana wa umoja wa mataifa Tanzania YUNA
Miongoni mwa wageni waliohudhuria na kuhutubia kongamano hilo ni pamoja na muhadhiri wa kimataifa na mkuu wa chuo cha sheria  nchini kenya profesa P.L.O Lumumba Ambaye pia aligusia suala la amani  barani afrika huku akikiri kuwa tatizo la afrika kwa sasa ni ukosefu wa ajira jambo ambalo huwafanya vijana wengi kujiunga na makundi ya kihalifu Lumumba liongeza kuwa vijana wananyimwa nafasi yakuhusishwa katika masuala ya uongozi na kusema kuwa ufisadi ni janga kubwa linalopelekea ukosefu wa ajira kwa vijana.
profesa P.L.O Lumumba

"Ufisadi ni janga kubwa barani Afrika na ndio hupelekea ukosefu na kufinywa kwa ajira mafisadi wanatakiwa kushughulikiwa kimagufuli" Lumumba aliongeza "siri ya maendeleo ni kuwa na vijana wenye siha njema na bongo kali"


Naye mgeni rasmi katika mkutano huo Brigedia Generali Ambasador Dr. wallace Williams alizungumzia suala la wakimbizi na kusema kuwa wakimbizi halali ni lazima wasaidiwe na washugulikiwe vizuri kwa sababu nji wa Afrika pia katika suala la elimu Brigedia Alipendekeza kuanzishwa shule za mitandaoni ambazo zitalenga kutoa elimu mkwa watu wa aina mbalimbali."kuanzishwa shule za mitandaoni naona litakuwa jambo sahihi kwa sababu itawasaidia watu wa bmatabaka mbalimbali" alisema Brigedia.
Brigedia Generaliamabsador Dr.wallace williams
mkutano huo mkubwa ambao huambatana na tuzo za watu waliofanya vizuri kwenye na kua na mchango mkubwa katika jamii ni watatu kufanyika na na hulenga kuangazia masuala ya amani na maendeleo barani Afrika zikianzia 2015 nchini ghana na kisha kufanyika nchini Dubai 2016 na 2017 umefanyika  humu nchini.
picha ya pamoja katika mkutano wa PanAfrica 2017 
Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka takriban nchi 27 za bara la Afrika ulikua na mijadala mbalimbali ambayo ilitoa nafasi na fursa kwa vijana kujifahamu na kujiinua kimaendeleo.kama vijana wa kitanzania natumai tumejifunza mengi katika mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here