Msemaji wa mashauri ya kigeni wa Korea Kaskazini ameviambia vyombo vya habari kuwa rais Trump ni muharibifu mkubwa wa dunia na anachochea vita na Korea Kaskazini.
Kwa mujibu wa habari,siku ya Jumatano Trump aliipa onyo kubwa Korea Kaskazini na kusema kuwa isidharau yale yanayoweza kufanywa na Marekani.
Kwa upande mwingine Korea Kaskazini imesema kuwa Trump anaasili ya kupenda vita vya makombora ya nyuklia.
Pyongyang imesema haibabaishwi na lolote na itazidi kutengeneza makombora ya nyuklia.



No comments:
Post a Comment