IJUE MIKOA INAYOONGOZA KUWA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, November 26

IJUE MIKOA INAYOONGOZA KUWA NA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

NA Anael James



Image result for glory mziray
Glory Mziray


MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini.
Alisema Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9.


Mwenyekiti mtendaji kutoka tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt  Fatma H. Mrisho akihutubia wakati wa mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi.
DK Fatma H Mrisho


Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Mikoa mingine aliyoitaja ni Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).

Mziray alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya Ukimwi yamepungua kwa kasi ndogo.

Alisema Watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.
Kuhusu tohara kwa wanaume, alisema inapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja ya kutoa elimu zaidi juu ya uelewa wa ugonjwa huo.
Visababishi vya Ukimwi:


Miongoni mwa vipengele muhimu ni pamoja na vifuatavyo:
Uasherati
Matumizi madogo na yasiyo endelevu ya kondomu
Ngono za marika yanayotofautiana sana
Kuwa na wapenzi wengi.
Ukosefu wa elimu ya maambukizo ya UKIMWI
Kuwepo kwa maradhi mengi ya ngono kama vile tutuko, homa,
Jando kwa wanaume
Sababu za mahali husika, za kushamiri kwa janga nchini ni:
Umaskini na biashara ya ngono pamoja na ongezeko la wafanyabiashara wa ngono
Tabia mbaya za ngono za wanaume kutokana na kuruhusiwa kimila kuwa na nguvu
Kukosekana usawa wa kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijinsia pamoja na unyanyaswaji wa wanawake na wasichana walio ndani na nje ya mahusiano.
Matumizi ya pombe na dawa za kulevya.

Tabia za kimila (kama vile utakasaji wajane na jando na unyago)
Safari za aina zote zinazosababisha kuwa mbali kwa wanandoa na ongezeko la mahawara na Kutokutahiriwa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here