Claudio afunguka kilichomtoa Barcelona - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, September 20

Claudio afunguka kilichomtoa Barcelona

Na Anael James Waziri_Tall


Golikipa namba moja wa Manchester City aliyejiunga na klabu hiyo msimu huu akitokea FC Barcelona ya Hispania Claudio Bravo Septemba 19 ameweka wazi kilichomuondoa FC Barcelona na kuamua kujiunga na Man City pamoja na kuweka wazi uhusiano wake na golikipa mwenzake Ter Stegen .
Bravo amezungumza kilichomuondoa FC Barcelona na kuamua kujiunga na Man City, kutokana na kutotaka kusaini mkataba mwingine FC Barcelona halafu aishie kukaa benchi, ni kweli uwepo wa Ter Stegen umemfanya aondoke FC Barcelona lakini sio kweli kama walikuwa na ugomvi na kipa huyo kama ambavyo inadaiwa na baadhi ya watu.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Claudio Bravo alijiunga na
Man City katika dirisha kubwa la usajili la majira ya joto mwaka huu 2016 na kurithi nafasi ya Joe Hart ambaye kocha
Pep Guardiola aliamua kumtoa kwa mkopo kwenda katika klabu ya Torino ya Italia .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here