Na Annael james
RAIS wa Olympique Lyon, Jean-Michel Aulas amedai meneja Bruno Genesio na
benchi lake la ufundi ndio walichukua uamuzi wa kumsajili Jean-Philippe Mateta
badala ya Emmanuel Adebayor.
ambaye ni mchezaji huru alikuwa akitegemewa kujiunga na klabu hiyo ya
Ligue 1 wiki iliyopita lakini dili hilo halikukamilika kama ilivyotarajiwa.
Lyon ilieleza sababu za kumuacha mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 32 kuwa ni
kukosekana kwake katika michuano ya Mataifa ya Afrika pamoja na kutoweza
kushiriki hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Aulas amesema Mateta mwenye umri wa miaka 19
ambaye amechukuliwa kutoka Chateauroux, alionyesha ni mtu sahihi kusajiliwa
kuliko mkataba wa kipindi kifupi ambao angepewa Adebayor.
Aulas amesema kutokana na kuumia kwa Alexandre Lacazette walikuwa wakitafuta
mchezaji wa safu ya ushambuliaji ili kuziba nafasi hiyo na walikuwa na machaguo
mengi kabla ya kocha na benchi lake kuamua kumchukua Mateta.
Post Top Ad
Responsive Ads Here
Author Details
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
No comments:
Post a Comment