Dodoma sasa hadi raha - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, September 20

Dodoma sasa hadi raha

Na Mustafa Ismail


Huku ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma umefikia asilimia 100, kumekuwa  na ongezeko la ndege zinazotua kila siku kutoka ndege tatu hadi kufikia tisa.

Akizungumza wakati wa mahojiano, Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, Julius Mlungwana ameisema kukamilika kwa ukarabati huo kutawezesha mashirika mengi ya ndege kuanza safari zake kuja Dodoma na hivyo kupunguza gharama za nauli.

Mlungwana alisema ukarabati huo umekamilika Septemba 2, mwaka huu na kina uwezo wa kuhudumua ndege zenye uwezo wa kubeba hadi abiria 90.
“Uwanja umekamilika kwa asilimia 100 kwa lengo la msingi na kilichobakia ni kuweka alama tu,” alisema meneja huyo na kuongeza kuwa kwenye usafiri wa anga kuna wadau wanaotumia kiwanja wakiwemo wafanyabiashara, wafanyakazi wa umma, mawakala wa utalii, taasisi za kimataifa na serikali, taasisi zisizo za kiserikali na wananchi.

“Hao wote wanatumia usafiri wa anga kilio chao kikubwa, nauli za ndege ni kubwa,” alisema na kuongeza kuwa kilio cha wadau kwenye usafiri wa anga ni gharama kubwa za usafiri kutokana na kuwepo kwa ndege mbili zilizo kwenye ratiba ya usafiri ambazo ni Auric Air na Flight Link ambazo zina uwezo wa kubeba abiria 13 kila moja.

“Pia kuna ndege zisizo na ratiba na za viongozi ambazo hazipo kwenye mpangilio pamoja na mashirika ya kimataifa ambao wamekuwa wakitumia ndege za kukodi,” alisema.
Naye Meneja Mradi wa Upanuzi wa uwanja huo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mbila Mdemu alisema mara ya mwisho ukarabati wa uwanja huo ulifanyika mwaka 1976, na 2005 ulifanyika upembuzi yakinifu kwa ajili ya ukarabati, lakini upatikanaji wa fedha umekuwa ni kikwazo na usanifu ukaishia kwenye ukarabati.

Alisema kutokana na agizo la Rais John Magufuli kuhamia Dodoma, uwanja ulianza kufanyiwa ukarabati.
Awali ujenzi ulitakiwa kukamilika ndani ya miezi sita na kuliwekwa malengo mawili ambapo ilitakiwa hadi Julai 20, mwaka huu kiwanja kiwe na uwezo wa kuhudumua ndege zenye uwezo wa kubeba abiria kati ya 70 na 90. Pia hadi Agosti 31, mwaka huu kazi za msingi zote ziwe zimekamilika na kazi zote zimefanikiwa kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here