Shamsa Ford aeleza jinsi walivyokutana na mpenzi wake Chidi Mapenzi - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, September 5

Shamsa Ford aeleza jinsi walivyokutana na mpenzi wake Chidi Mapenzi

Na Babu Ally

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford ambae amefunga ndoa wiki iliyopita na mfanya biashara Chidi Mapenzi amefunguka na kusema jinsi walivyokutana na mpenzi wake huyo.



Shamsa ford anasema kuwa siri ya mahusiano aijuae ni Mungu kwani yeye alikuwa anapita karibu kila siku kwenye duka la nguo la Chidi Mapenzi tena bila hata kusalimia kumbe huyo mtu ambaye anampita kila siku ndiye mume aliyeandaliwa na Mungu.

"Kiukweli siri ya mahusiano aijuae ni Mungu. Nilikuwa napita tu ofisini kwako tena bila hata salamu, nakumbuka siku niliyokuwa nakula karibu na ofisi yako kwa bahati mbaya chakula kilinimwagikia kwenye nguo na ikanibidi niingie ofisini kwako ili niweze kununua nguo mpya. Daa kumbe Mungu alikuwa ananikutanisha na mume wangu kipenzi jamani. Asante Mungu kwa mume bora uliyenipa. Muda wa Mungu ndiyo muda sahihi"alisema Shamsa Ford

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here