ZOEZI LA WASANII KUCHUKUA FUMU ZA EATV AWARDS LIMEFUNGULIWA RASMI LEO - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, September 13

ZOEZI LA WASANII KUCHUKUA FUMU ZA EATV AWARDS LIMEFUNGULIWA RASMI LEO

Na Babu Ally

Zoezi la wasanii kuchukua fomu za kushiriki kwenye tuzo za mwaka huu za EATV limefunguliwa Jumanne hii.

 
Akiongea kupitia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Mkuu wa Masoko wa EATV, Roy Mbowe alisema mwisho wa kuchukua fomu na kuzirudisha ni Oktoba 22 saa 11 jioni.
Amesema fomu zinaweza kujazwa na msanii mwenyewe au meneja wake, lakini pia lazima kuwepo na mashahidi watakaojaza pia. Wasanii watatakiwa kuzirudisha fomu hizi pamoja na kazi zao.
Fomu hizo zinapatikana kwenye tovuti ya http://www.eatv.tv/awards
Tuzo hizo zitakuwa na vipengele 10 zitakazohusisha muziki, filamu na tuzo moja ya heshima.
Vipengele hivyo ni:
1. Mwanamuziki bora wa kiume
2. Mwanamuziki bora wa kike
3. Mwanamuziki bora chipukizi
4. Kundi bora la muziki
5. Video bora ya muziki
6. Wimbo bora wa mwaka
7. Muigizaji bora wa kiume
8. Muigizaji bora wa kike
9. Filamu bora ya mwaka
10. Tuzo ya heshima itakayotolewa kwa mtu au kampuni iliyochangia kwa kiasi kikubwa katika kazi za muziki.
Tuzo hizo zinazodhaminiwa na kampuni ya Vodacom, zitatolewa December 10 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here