Na Anael James
WINGA wa klabu ya Genk, Leon Bailey amesisitiza kuwa
atakataa nafasi ya kusaini Manchester United kama timu hiyo haitamuhakikishia
nafasi ya kuwepo katika kikosi cha kwanza.
Chipukizi huyo wa kimataifa wa
Jamaica mwenye umri wa miaka 19, anatajwa kama mmoja wa wachezaji wanaovutia
nchini Ubelgiji na amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na klabu kubwa.
Paris Saint-Germain-PSG na Ajax Amsterdam zote zinatajwa kuwa zilijaribu
kumsajili majira ya kiangazi wakati United nao pia wanaaminika kumfuatilia kwa
karibu chipukizi huyo.
Lakini Bailey mwenyewe ameweka wazi kuwa hana haraka
yeyote ya kuondoka Genk kwasasa na kama akiondoka basi atakwenda katika klabu
itakayoweza kumuhakikishia naafsi ya kucheza.
Bailey amefunga mabao nane katika
mechi 25 za mashindano yote alizocheza msimu huu.
No comments:
Post a Comment