COUTINHO ATAKIWA CAMP NOU _ BARCELONA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Saturday, November 12

COUTINHO ATAKIWA CAMP NOU _ BARCELONA


NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL

KLABU ya Barcelona inadaiwa kumuweka nyota wa Liverpool Philippe Coutinho katika orodha yao ya juu ya usajili ujao. 
 LIVERPOOL, ENGLAND - NOVEMBER 06:  (THE SUN OUT, THE SUN ON SUNDAY OUT) Philippe Coutinho shows his appreciation to the fans during the Premier League match between Liverpool and Watford at Anfield on November 6, 2016 in Liverpool, England.  (Photo by John Powell/Liverpool FC via Getty Images)
Kiungo huyo wa kushambulia amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu na kufanya vilabu vingi kuanza kummezea mate wakiwemo mahasimu wa Barcelona Real Madrid. 

Coutinho amekuwa na urafiki wa karibu na nyota wa Barcelona Neymar huku pia wakionekana kuelewana sana pindi wanapokutana katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil. 

Nyota hao wawili wote walifunga mabao katika ushindi mnono wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Argentina katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia kwa nchi za Amerika Kusini jana alfajiri. Taarifa zinadai kuwa Barcelona wako tayari kutoa kitita cha paundi milioni 65 kwa ajili ya nyota huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here