Yajue mambo matano makubwa aliyoyafanya Magufuli ndani ya mwaka 1 - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, November 4

Yajue mambo matano makubwa aliyoyafanya Magufuli ndani ya mwaka 1

Na Mustafa Ismail
Ikiwa ni mwaka mmoja tangu  Rais John Magufuli kuingia madarakani kuna mambo mbalimbali ameyafanya yanaweza kutajwa kuwa yametikisa Taifa na ulimwenguni kwa jumla  katika utawala wake
Mambo hayo kati ya mengi yamelitikisa Taifa kwa nyaja tofauti kutokana na kasi ya Rais Magufuli kiutendaji, huku baadhi ya watu wakifurahia hatua hizo na wengine kuumia na kunung’unika kwa kuguswa katika maeneo yao ya utendaji.
Kufuta safari za nje, kufuta sherehe za kimataifa, kutangaza serikali kuhamia Dodoma, kuondoa watumishi hewa, elimu bure.
Kuzuia mikutano ya siasa kutumbua watendaji wa serikali na taasisi zake na zile za umma.
  1. WATUMISHI HEWA-alitangaza mpango wa kuondoa watumishi hewa siku ya maadhimisho ya wafanyakazi,alibainisha watumishi hewa 10,295 serikalini kati yao watumishi hewa 8,373 wametoka Tamisemi na 1,922 wanatoka serikali kuu
  2. KUFUTA SHEREHE-Novemba 8 mwaka jana, ikiwa siku 3 baada ya kuapishwa alitangaza kuokoa sh. Milioni 225 zilizochangwa kugharamia hafla ya wabunge na kuagiza zinunulie vitanda kwa ajili ya hospital ya Taifa Muhimbili.
  3. KUFUTA SAFARI ZA NJE-Novemba 7 mwaka jana Rais alitangaza kufuta safari za nje ya nchi kwa viongozi wa serikali, wa ngazi zote hadi mawaziri, watakaosafiri kwa kibali maalumu.
  4. KUHAMIA DODOMA-Rais Magufuli alitoa kauli ya kutaka serikali kuhamia Dodoma huku akisisitiza atahakikisha serikali yote inahamia mkoani humo kufikia mwaka 2020.
5.KUFUFUA SHIRIKA LA ATCL-kwa kununua ndege mbili mpya
Kubwa zaidi ni kompongeza rais magufuli na kushikiana katika kuleta maendeleo ndani ya nchi yetu.tunachotakiwa kuacha ni tofauti za kisiasa,kikabila na kidini ili tufikie malengo ya serikali ya tano lakini pia malengo ya watanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here