Na Anael James
KIUNGO wa Real Madrid, Isco amedai kutaka kuongeza mkataba
mpya na klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu.
Nyota huyo amewahi
kukaririwa kipindi cha nyuma akidai kuwa anaweza kuondoka Madrid ili aweze
kupata nafasi zaidi ya kucheza seemu nyingine lakini katika wiki za karibuni
ameimarika na kuwa mchezaji muhimu katika timu hiyo.
Isco mwenye umri wa miaka
24 ameeleza kufurahishwa kwake na maendeleo yake na sasa anataka kuongeza
mkataba mwingine na klabu hiyo.
Akihojiwa Isco ambaye alikuwa akihusishwa na
tetesi za kutakiwa Tottenham Hotspurs, amesema bado ana mkataba wa mwaka mmoja
na nusu na Madrid lakini yeye pamoja na klabu wanataka kuongeza mkataba hivyo
ana matumaini kila kitu kitakwenda sawa.
Isco aliendelea kudai kuwa kwasasa
anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo anafurahia kwani anaisaidia timu.
No comments:
Post a Comment