ROONEY KUTUPWA NJE ENGLAND KESHO - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, November 14

ROONEY KUTUPWA NJE ENGLAND KESHO

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL



JUMANNE Usiku England watacheza Mechi ya Kimataifa ya Kirafiki Uwanjani kwao Wembley Jijini London dhidi ya Spain na Kepteni wao Wayne Rooney hataanza Mechi hii.
Image result for ROONEY
Kwa mujibu wa Kocha wa Muda wa England, Gareth Southgate, hatamuanzisha Rooney na Utepe wa Unahodha utavaliwa na Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson.
Henderson, Mwenye Miaka 26, alikuwa ndie Nahodha wa England walipotoka Sare  0-0 Ugenini na Slovenia Mwezi uliopita wakati Rooney alipoanzia Benchi.
Hii Leo, Rooney, ambae Ijumaa aliiongoza Timu yao kuitandika 3-0 Scotland katika Mechi ya Kundi ya kusaka kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia, hakufanya Mazoezi na Kikosi cha England ikisemekana ana maumivu kidogo.
Hapo Kesho Jumanne zipo Mechi nyingi za Kimataifa za Kirafiki na zamvuto ni pamoja na Italy kucheza na Mabingwa wa Dunia Germany na France kuwavaa Mabingwa wa Afrika Ivory Coast huko Stade Bollaert-Delelis, Mjini Lens Nchini France.

Mechi za kesho Jumanne


 Novemba 15

14:00 Jordan v Lebanon             
14:00 Bahrain v Kyrgyzstan                  
16:00 Kenya v Liberia                
17:00 Morocco v Togo                
17:00 Tunisia v Mauritania                   
17:00 Gabon v Comoros             
18:00 Tunisia v Mauritania                   
19:00 Russia v Romania             
21:00 Malta v Iceland                
21:45 Hungary v Sweden          
22:00 Ukraine v Serbia               
22:30 Czech Republic v Denmark                   
22:45 Northern Ireland v Croatia          
22:45 Italy v Germany               
22:45 Austria v Slovakia             
23:00 France v Ivory Coast                  
23:00 England v Spain
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here