ANGALIA MAN UNITED WANAVYO ONGOZA KULIPWA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, November 14

ANGALIA MAN UNITED WANAVYO ONGOZA KULIPWA




 NA ANAEL JAMES WAZIRITALL

WACHEZAJI wa Manchester United ndio wanaolipwa zaidi katika soka duniani lakini wako nyuma ya mabingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani-NBA, Cleveland Cavaliers.
 Image result for MANCHESTER UNITED

 Kwa mujibu wa jarida moja la uchunguzi wa mishahara la GSSS,United wanashikilia nafasi ya nne kwa mwaka huu. Klabu hiyo ya Ligi Kuu imetoka katika nafasi ya sita walipokuwa awali baada ya makadirio ya mishahara kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza kufikia paundi milioni 5.77 kwa mwaka. Hata hivyo bado wameachwa nyuma na Cavaliers ambao makadirio yao kwa mwaka ni paundi milioni 6.54 wakifuatiwa na New York Yankees ya Baseball wanaolipa paundi milioni 5.81 huku Los Angeles Clippers wakikadiriwa kulipa paundi milioni 5.78 kwa mwaka. Mabingwa wa La Liga Barcelona wanaokadiriwa kulipa paundi milioni 5.64 na Manchester City paundi milioni 5.42 ndio klabu pekee za soka zilizopo katika orodha 10 bora. NBA imeingiza timu 14 katika orodha ya timu 20 bora.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here