Wanafunzi kadha wa shule moja eneo la Sichuan, China wamepata ngazi mpya kuwasaidia kupanda na kushuka urefu wa mita 800 kufika na kuondoka shule.
Kijiji cha Atuler kimepewa jina la utani "kijiji cha mwamba". Kijiji hiki hupatikana mita 800 juu kwenye nyika eneo la Sichuan, China. Wanaoishi hapa ni watu wa ya Yi, ambao pia hupatikana Vietnam na Thailand.
Hadi kufikia sasa, kulikuwa na ngazi 17 za mbao ambayo ilikuwa njia pekee ya wakazi wa kijiji hiki kutoka nje ya kijiji chao. Kupanda ngazi hizi lilikuwa jambo hatari na watu zaidi ya saba walifariki wakizikwea, wakazi wanasema.
sasa, ngazi ya chuma imejengwa kurahisisha safari yao. Lakini bado ni shughuli hatari, ingawa muda wanaotumia kupanda na kushuka umepungua.
watu wa jamii ya Yi wanaoishi Atuler wamekuwa wakikwea mwamba huo kwa miaka na mikaka na wana hata kanuni za kupanda. Wakati wa kupanda, wanaume wanawajibika kuwabeba na kuwatunza watoto. Watoto wa chini ya miaka 16 hawaruhusiwi kupanda au kushuka kwenye ngazi hiyo wakiwa peke yao.
gazi hiyo ya chuma ilijengwa baada ya habari za kijiji hicho kugonga vichwa vya habari kimataifa mwezi Mei. Ingawa wengi wanasifu ujenzi wa ngazi hiyo, wapo watu wanaoshangaa ni kwa nini wanakijiji hao hawawezi kuhamia eneo linalofikiwa kwa urahisi. Lakini wakazi waliambia wanahabari CHina kwamba hawataki kuacha nyumba zao, hasa kuhamia mijini ambapo maisha wanaamini ni magumu sana.
No comments:
Post a Comment