STEVEN GERRAD RASMI ASTAAFU SOKA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, November 24

STEVEN GERRAD RASMI ASTAAFU SOKA

NA Anael James
NAHODHA wa zamani wa Liverpool na England Steven Gerrard ametangaza rasmi kustaafu kucheza Soka la Kulipwa.

Image result for steven gerrard

Gerrard alianza Soka lake huko Liverpool tangu Utoto wake na kuibuka kuwa Kepteni wao wa muda mrefu kabisa katika Historia ya Klabu ambayo aliichezea Mechi 710 na kuiwezesha kutwaa Ubingwa wa Ulaya Mwaka 2005 pamoja na FA CUP mara 2 Miaka ya 2001 na 2006, Kombe la Ligi mara 3, Miaka ya 2001, 2003 na 2012 na UEFA CUP 1 Mwaka 2001 katika himaya yake ya Miaka 18 huko Anfield.
Kwenye Timu ya Taifa ya England, Gerrard aliichezea Mechi 114 na yeye ni Mchezaji wa 4 wa Nchi hiyo kuichezea Mechi nyingi akitanguliwa tu na Peter Shilton, Wayne Rooney na David Beckham.
Image result for steven gerrard

Gerrard aliiongoza England kama Nahodha kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 na 2014 na pia EURO 2012.
Baada ya kuacha kuichezea Liverpool, Gerrard alihamia huko USA Mwaka 2015 kwenda kuichezea Klabu ya LA Galaxy na sasa, akiwa na Miaka 36, ameamua kabisa kustaafu Soka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here