TAIFA STARS YAPEWA DOZE TAMU - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, November 13

TAIFA STARS YAPEWA DOZE TAMU

NA ANAEL JAMES WAZIRI_TALL

Tanzania wakiwa chini ya kocha wao mkuu Charles Boniface Mkwasa na nahodha wao Mbwana Samatta walikubali kupoteza kwa jumla ya goli 3-0, Zimbabwe ambao waliutawala mchezo kwa kiasi kikubwa walipata goli la kwanza dakika ya 9 kupitia kwa mshambuliaji wao anayecheza KV Oostende ya Ubelgiji Knowledge Musona.


  

Mchezo ulienda mapumziko Zimbabwe wakiwa mbele kwa goli 1-0, lakini kipindi cha pili Zimbabwe wakarudi na mpango mpya uliowasaidia kufunga magoli mawili dakika ya 54 kupitia kwa Mathew Rusike na Nyasha Mushekwi dakika ya 57.

Zimbabwe wanaonekana kuwa imara zaidi ya Tanzania kwani wapo nafasi ya 110 katika viwango vya FIFA na Tanzania wapo nafasi ya 144, kwa mechi 12 zilizopita Tanzania alikuwa kapoteza mechi 5 huku akisha mechi 2 na kutoka suluhu mechi 5.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here