wakenya waandamana kupinga ufisadi - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, November 4

wakenya waandamana kupinga ufisadi

Na Mustafa Ismail
Kenya
Mamia ya watu wamekusanyika eneo la Freedom Corner katika Uwanja wa Uhuru Park, katikati mwa jiji la Nairobi, kuandamana kulalamikia wanachosema ni ongezeko la visa vya ufisadi serikalini.
baadhi wa waandamani wakiwa wamebeba mabango mbalimbali




baadhi ya waandamanaji wakiwa maejifunga minyororo

Maandamano hayo yanafanyika siku chache baada ya gazeti moja kuchapisha habari zinazodai jumla ya dola 50 milioni za Marekani katika wizara ya afya zilitumiwa vibaya au zikaporwa

Wanaharakati walioandaa maandamano ya leo wanamtaka Rais Uhuru Kenyatta achukue hatua la sivyo ajiuzulu.
Polisi wametumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya.
polisi wakiwatawanya waandamanaji kutumnia mabomu ya machozi
 Ufisadi umekuwa changamoto kubwa na donda sugu si tu nchini kenya bali ulimwengu kwa ujumla huku kidole cha lawama kikielekezwa kwa serikali kwa kulifumbia macho swala hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here