KADI NYEKUNDU ALIYOPEWA JAMIE VARDY YAWA GUMZO,HABARI ZAIDI HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Monday, December 19

KADI NYEKUNDU ALIYOPEWA JAMIE VARDY YAWA GUMZO,HABARI ZAIDI HAPA

Image result for leicester city
WAKATI Klabu Bingwa ya England Leicester City ikiwa mbioni kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Straika wao Jamie Vardy, FIFA imezitwanga Faini FA za England, Scotland, Wales na Northern Ireland kwa kuvaa Utepe wa Maua Mkononi wakati wa Mechi zao Mwezi uliopita.

LEICESTER CITY KUKATA RUFAA KADI NYEKUNDU YA JAMIE VARDY
Leicester City wapo mbioni kukata Rufaa kupinga Kadi Nyekundu ya Straika wao ambae pia anachezea England, Jamie Vardy, aliyopewa Jumamosi wakitoka Droo ya 2-2 na Stoke City.
Vardy alionyeshwa Kadi Nyekundu na Refa Craig Pawson kwa kumrukia Miguu miwili Mame Diouf.
Lakini Leicester inataka kupeleka utetezi kuwa Vardy alisukumwa na ndio maana akatua kwa Miguu Miwili na hakukusudia kutenda hiyo Rafu.
FA, Chama cha Soka cha England, kinatarajiwa kuishushia Leicester Faini kwa vile Refa Pawson aliwapa Kadi za Njano Wachezaji Watano wa Timu hiyo mwishoni mwa Kipindi cha Kwanza na mpaka mwisho wa Mechi hiyo na Stoke Kadi zilishushwa kwa Wachezaji wao 6.
Kanuni za FA zinatamka kuwa Timu inapigwa Faini moja kwa moja ikiwa Wachezaji wao 6 au zaidi watapewa Kadi za Njano.
Miongoni mwa waathirika wa Kadi hizo ni Robert Huth na Christian Fuchs ambao sasa wamelimbikiza Jumla ya Kadi za Njano 5 na sasa watakuwa Kifungoni Mechi 1 na kuikosa Mechi ya Leicester na Everton hapo Desemba 26.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here