MNYAMA SIMBA SC AUNGURUMA KILELENI VIONGOZI WAZUNGUMZA,SOMA HAPA ZAIDI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, December 18

MNYAMA SIMBA SC AUNGURUMA KILELENI VIONGOZI WAZUNGUMZA,SOMA HAPA ZAIDI

Image result for simba sc
Mchezo uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu kama Mnyama Simba SC ataweza kurudi kileleni mwa ligi hatimaye umekamilika kwa Wekundu wa msimbazi kutoka na point 3 muhimu siku ya leo kule Nangwanda Sijaona.
Magoli ya Mzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim yameirejesha tena Simba katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuifunga Ndanda FC kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Mzamiru alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 64 kabla ya Mohamed Ibrahim ‘MO’ kuihakikishia Simba ushindi na kuendeleza ubabe dhidi ya Ndanda FC.
Simba imerejea kwenye nafasi yake baada ya jana (Jumamosi December 17) Yanga kushinda mchezo wake dhidi ya JKT Ruvu na kukaa kileleni mwa VPL kwa muda ikisubiri matokeo ya Ndanda vs Simba.
Ushindi wa Simba unaifanya kufikisha pointi 38, pointi mbili mbele ya Yanga huku timu zote zikiwa zimecheza mechi sawa hadi sasa (16).
kwa upande wa historia ya Wekundu hao wa Msimbazi na Wanakuchele tangu mwaka 2015 ipo hivi.......
Simba haijawahi kupoteza pointi hata moja dhidi ya Ndanda tangu Ndanda ilivyopanda kucheza ligi kuu Tanzania bara.
18/12/2016 Ndanda FC 0-2 Simba
20/08/2016 Simba 3-1 Ndanda FC
10/03/2016 Simba 3-0 Ndanda FC
01/01/2016 Ndanda FC 0-1 Simba
25/04/2015 Simba 3-0 Ndanda FC
17 01/2015 Ndanda FC 0-2 Simba
Ndanda FC haijawahi kuifunga Simba wala kutoka sare tangu imepanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara, imefungwa mechi zote za nyumbani na ugenini.
Simba ilihitaji matokeo ya ushindi pekee ili kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi. Endapo Simba ingepata matokeo ya sare/suluhu au kufungwa, ingesalia nafasi ya pili na Yanga ingeendelea kuongoza kwa sababu Yanga ina uwiano mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa ukilinganisha na Simba.
Simba imekuwa timu pekee msimu huu ambayo imetibua rekodi zilizokaribia kuwekwa na Stand United na Ndanda kwa kuzibania ushindi timu za Dar zenye majina makubwa.
Stand United ilizifunga Yanga na Azam kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga lakini ikakubali kichapo kutoka kwa Simba.
Ndanda ilitoka suluhu na Yanga halafu ikaifunga Azam kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara lakini wamekubali kipigo cha Simba.
Upande wa viongozi wa timu wamezungumza kuwa Simba ya sasa imejipanga kuhakikisha inachukua ubingwa wa ligi kwa udi na uvumba na mechi zote itakuwa ni fainali upande wa wekundu wa msimbazi.
Matokeo ya leo kwa mechi zingine
Mbao FC 1-0 Stand United
African Lyon 0-0 Azam FC
Tanzania Prisons 1-0 Majimaji FC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here