KIKOSI CHA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA SC TAYARI KIMEKWEA MTWARA NA KIKOSI KIPYA,HABARI ZOTE HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, December 15

KIKOSI CHA WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA SC TAYARI KIMEKWEA MTWARA NA KIKOSI KIPYA,HABARI ZOTE HAPA

 Image result for SIMBA SC
KIKOSI cha wekundu wa msimbazi Simba SC kimeondoka leo asubuhi Dar es Sakaam kwenda Mtwara tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
  Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, Hajji Sunday Manara ameiambia MKWELITZ BLOG leo kwamba timu imeondoka na wachezaji  20 kwa ajili ya mchezo huo.


Simba watakuwa wageni wa Ndanda FC Jumapili Uwanja wa Nangwanda, Sijaona, Mtwara katika fungua dimba ya duru la pili la Ligi Kuu.
KIKOSI cha Simba kimeondoka leo asubuhi Dar es Sakaam kwenda Mtwara tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
 
 
Na ingawa Manara hakutaja wachezaji walioongozana na timu mjini humo, lakini MKWELITZ BLOG inafahamu ambao hawajakwenda kwa sababu mbalimbali ni Juuko Murshid, Mwinyi Kazimoto, Mussa Ndusha, Pastory Athanas, Emmanuel Semwanza na kipa Vincent Angban.

  Muivory Coast Angban na Ndusha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wanaachwa baada ya kusajiliwa wachezaji wapya kutoka Ghana, kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei.
  Murshid bado yuko na timu yake ya taifa ya Uganda, Mwinyi Kazimoto ni majeruhi, Pastory Athanas hajakamilisha uhamisho wake kutoka Stand United na Emmanuel Semwanza ana matatizo ya kifamili.
  Wachezaji wanaotarajiwa kuwamo kwenye msafara ni makipa; Daniel Agyei, Peter Manyika, mabeki; Hamad Juma, Janvier Bokungu, Abdi Banda, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga na Method Mwanjali.
  Viungo ni James Kotei, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Muzamil Yassin, Jamal Mnyate, Shizza Kichuya na washambuliaji Frederick Blagnon, Laudit Mavugo, Ame Ally na Ibrahim Hajib, Juma Luizio na Hajji Ugando. Simba ilimaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika nafasi ya kwanza kwa pointi zake 35, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here