LIGI KUU KUENDELEA KESHO TENA,ANGALIA HAPA RATIBA ZOTE HADI MWEZI JANUARI - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, December 27

LIGI KUU KUENDELEA KESHO TENA,ANGALIA HAPA RATIBA ZOTE HADI MWEZI JANUARI

Image result for vodacom premier league tanzaniaMABINGWA Watetezi Yanga Jumatano wako Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kucheza na Ndanda FC katika Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom.
 
Mechi hiyo itawafanya Yanga, ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 4 nyuma ya Vinara Simba, kusaka ushindi ili kulikata pengo hilo baada ya Wiki iliyopita kuzimwaga Pointi 2 kwa suluhu na African Lyon.


Hivi sasa Ndanda FC wapo Nafasi za chini wakiwa Pointi 18 nyuma ya Yanga.

Mechi nyingine Jumatano ni kati ya Mtibwa Sugar na Majimaji FC huko Manungu, Morogoro.

Alhamisi pia zipo mechi 2 na moja ipo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kati ya Ruvu Shooting na Simba na nyingine ni pia Jijini Dar es Salaam huko Azam Complex kati ya Azam FC na Tanzania Prisons.


Jumatano Desemba 28

Yanga v Ndanda FC [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]
Mtibwa Sugar v Majimaji FC [Manungu, Manungu]

Alhamisi Desemba 29

Ruvu Shooting v Simba [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]
Azam FC v Tanzania Prisons [Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam]

Jumamosi Desemba 31

Mwadui FC v Kagera Sugar [Mwadui Complex, Mwadui]
African Lyon v JKT Ruvu [Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam]
Mbeya City v Mbao FC [Sokoine, Mbeya]

Jumapili Januari 1

Toto African v Stand United [CCM Kirumba, Mwanza]

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here