SIMBA YASAJIRI KIFAA KINGINE,HABARI ZOTE NA MKWELITZ BLOG - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, December 14

SIMBA YASAJIRI KIFAA KINGINE,HABARI ZOTE NA MKWELITZ BLOG

Klabu ya Simba imemsajili mshambuliaji nyota wa Stand United anayejulikana kwa jina la  Pastory Athanas.

Athanas amesaini mkataba wa miaka miwili leo mbele ya Rais wa Simba, Evans Aveva.

Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon, mara baada ya mzunguko wa kwanza kwisha, kwenye ripoti yake aliutaka uongozi kumsajili mshambuliaji mkali atakayesaidiana na Laudit Mavugo raia wa Burundi na Frederci Blagnon.


Athanas ambaye ana umri wa miaka 22 kama ilivyoelezwa ni mmoja wa washambuliaji hatari walioshiriki Ligi Daraja la Kwanza na imeelezwa alifanya vema katika misimu miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here