Kamishna Simon Sirro amjibu Mzee wa Upako juu ya kuwatishia amani waandishi wa habari kuwa watakufa wale walio andika habari ya kumchafua - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, December 14

Kamishna Simon Sirro amjibu Mzee wa Upako juu ya kuwatishia amani waandishi wa habari kuwa watakufa wale walio andika habari ya kumchafua

Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo. 

Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani. 

  ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana  alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo. 

“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.

 Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here