YANGA SC YAMSAJIRI MZAMBIA DAKIKA ZA MWISHO NA CHIRWA KUTUPWA KWA MKOPO,HABARI ZOTE HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Friday, December 16

YANGA SC YAMSAJIRI MZAMBIA DAKIKA ZA MWISHO NA CHIRWA KUTUPWA KWA MKOPO,HABARI ZOTE HAPA


Yanga imefanikiwa kupitisha jina la mshambuliaji wa zamani wa Zesco, Winston Kalengo.

Kalengo ametua Yanga baada ya jina lake kuwasilishwa katika nusu saa ya mwisho kabla ya dirisha ya usajili.

Taarifa zinaeleza, Yanga imepitisha jina hilo la Kalengo anayechukua nafasi ya Mzambia, Obey Chirwa.

Yanga imemrudisha Chirwa FC Platnums kwa mkopo, safari hii akiwa analipwa nusu mshahara na Yanga na Wazimbabwe hao watamlipa nusu mshahara.


Mjadala mkubwa kuhusiana na hilo, ndiyo ulichelewesha Yanga kuwasilisha jina hilo katika hatua za mwisho na imeelezwa Yanga wameliwasilisha katika majina ya wachezaji wao saa 5:36, ikiwa ni dakika 24 kabla ya usajili huo wa dirisha dogo kufungwa.

Pamoja na kufanya vizuri Zambia akiwa na Zesco, Kalengo aliwahi kucheza soka la kulipwa nchini Congo Brazaville na anaelezwa kuwa mkali wa kupiga mashuti, mwenye njaa ya mabao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here