RONALDO AFUNGA GOLI LA 500 MADRID WAKITINGA FAINAL LEO,HABARI ZOTE HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, December 15

RONALDO AFUNGA GOLI LA 500 MADRID WAKITINGA FAINAL LEO,HABARI ZOTE HAPA

 

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo mapema leo amefunga bao lake la 500 kwa klabu katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Club America kwenye michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia. 

Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, alifunga bao lake la 500 kwa klabu na nchi yake katika mchezo dhidi ya Malmo Septemba mwaka jana na sasa amefikisha bao la 500 kwa klabu pekee. 

Nyota huyo alifunga bao hilo katika dakika 90 ya mchezo akiwahadaa walinzi wa America lakini ilibidi asubiri mwamuzi Enrique Caceres wa Venezuela kwenda kuangalia upya kama alikuwa kaotea kupitia mfumo mpya wa picha za video wa VAR unaotumika kwenye michuano hiyo. 

Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye alijiunga na Madrid kwa ada iliyovunja rekodi mwaka 2009, amefunga bao lake la 500 katika mechi 689 pekee alizocheza. 

Ronaldo alifunga bao lake la 377 katika mechi 367 na pia alifunga mabao 118 katika mechi 292 alizoichezea Manchester United na matano katika mechi 31 alizocheza Sporting Lisbon.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here