Winga huyo wa zamani wa Manchester United amekiri makosa mawili tofauti ya ukwepaji kodi, ambalo kila moja amepewa kifungo cha miezi sita jela.
Akiwa anachezea Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa sasa, Di Maria alikutwa na hatia na Serikali ya Hispania, ya kutolipa kodi kiasi cha Pauni Milioni 1.14 wakati anacheza Real Madrid kuaniza mwaka 2010 hadi 2014.
Pamoja na hayo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hatakwenda jela, kwa sababu nchini Hispania kifungo cha chini ya miaka miwili kwa mtu anayetiwa hatiani kwa kosa la kwanza hupewa kifungo cha nje.
Awali, Murgentina huyo alikubaliana na mamlaka ili kukwepa adahbu zaudui za Makahama Kuu ya Hispania.
Mwaka jana, Lionel Messi alikutwa na makosa ya kukwepa kodi pia kwa pamoja na baba yake, lakini pamoja na nyota huyo wa Barcelona kuhukumiwa kifungo cha miezi 21 jela, lakini hakwenda jela.
Wakati huo huo Jose Mourinho naye yuko matatani na Mamlaka ya Kodi ya Hispania akipinga shutuma dhidi yake kwa kudai alilipa Euro Milioni 26 kati ya mwaka 2010 na 2013.
Manchester United imeamua kushikamaan na kocha waobaada ya kudaiwa amekwepa kodi kiasi cha Euro Milioni 3.3.
Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo ambaye amekuwa anacheza Real Madrid tangu wakati wa Mourinho naye anadaiwa kukwepa kodi pia kiasi cha Pauni Milioni 12.9.
No comments:
Post a Comment