Ngogo ambaye ni Mkazi wa Tabata Segerea amefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa na kusomewa mashitaka yake na Inspekta msaidizi wa polisi Hamisi Saidi.
Imedaiwa kuwa, Juni 15, mwaka huu maeneo ya bandari kavu ya Galco iliyopo Chang'ombe wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Ngogo alikutwa na suruali 5,000 za JWTZ kwenye kontena namba PCIU 82851 (5) zenye thamani ya Sh milioni 59 mali ya serikali bila kuwa na kibali.
Hata hivyo, mshtakiwa amekana mashtaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamama.
Akisoma masharti hayo ya dhamana, Hakimu Nongwa amemtaka mshitakiwa kuwasilisha fedha taslimu milioni 30 au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo pamoja na wadhamini wawili watakaosaini ahadi ya milioni 10 kila mmoja.
Kesi imeahirishwa hadi Julai 17 mwaka huu itakapokuja kwa kutajwa. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi bado haujakamilika
No comments:
Post a Comment