Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema tayari serikali imetoa kibali cha ajira 15,000 kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliofutwa kazi baada ya waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi katika kada mbalimbali.
Waziri Kairuki ameyasema hayo leo bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati aliyetaka kujua mpango wa serikali kuhusu kujaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi wa umma walioacha kazi kufuatia agizo la Rais Magufuli alilolitoa mapema Mei mwaka huu.
Waziri Kairuki alisema kuwa ni kweli baada ya watumishi hao kuondoka katika vituo vyao vya kazi, sehemu mbalimbali zilikumbwa na uhaba wa watumishi na hivyo kupelekea kuzorota kwa utoaji wa huduma. Lakini ili kukabailiana na hilo, hivi karibuni serikali imetoa kibali cha kuajiri watumishi wapya kujaza nafasi hizo.
Mei mwanzoni Rais Magufuli aliagiza hadi Mei 15 mwaka huu watumishi wote waliotajwa katika orodha ya wenye vyeti vya kughushi waondoke mara moja la si hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment