Uganda na Nepal zaanzisha uhusiano wa kibalozi - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Tuesday, June 13

Uganda na Nepal zaanzisha uhusiano wa kibalozi


Wizara ya Mambo ya Nje ya Nepal imesema, nchi hiyo na Uganda zimeanzisha rasmi uhusiano wa kibalozi hii leo.

Wizara hiyo imesema, Balozi wa kudumu wa Nepal katika Umoja wa Mataifa Durga Prasad Bhattarai na balozi wa kudumu wa Uganda katika Umoja huo Adonia Ayebare wamesaini taarifa ya pamoja katika hafla fupi iliyofanyika mjini New York, Marekani.

Katika hafla hiyo, mabalozi hao walieleza matumaini yao kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo kutazileta nchi hizo mbili karibu zaidi katika jukwaa la pande nyingi na kusaidia ushirikiano wa karibu zaidi wa pande mbili. Pia kubadilishana uzoefu katika kutafuta maendeleo na amani kwa nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here