KLABU ya
Barcelona jana imeweka historia mpya ya kuwa timu ya kwanza kucheza pasi nyingi
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana.
Wakiwa
tayari wameshafuzu wakiwa vinara w akundi C, Barcelona walishinda mabao 4-0
dhidi ya Borussia Monchengladbach, mabao yaliyofungwa na Lionel Messi na Arda
Turan aliyefunga hat-trick.
Katika
mchezo huo Barcelona walicheza pasi 993 ikiwa ni nyingi zaidi kuliko timu
yeyote toka rekodi hizo zilipoanza kutunzwa katika msimu wa 2003-2004.
Mapema msimu
huu, kipa wa Barcelona Marc-Adre ter Stegen aliweka rekodi mpya katika La Liga
baada ya kutoa pasi zilizokamilika 51 kati ya 62 alizopiga dhidi ya Athletic
Bilbao.
No comments:
Post a Comment