FRANK LAMPARD APATA ULAJI TIMU YA TAIFA UINGEREZA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Wednesday, December 7

FRANK LAMPARD APATA ULAJI TIMU YA TAIFA UINGEREZA

Image result for lampard
KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Chelsea, Frank Lampard anatarajiwa kupewa nafasi katika benchi la ufundi la timu ya taifa ya Uingereza.

Taarifa hizo za kocha mpya wa Uingereza Gareth Southgate kumtaka Lampard zimekuja saa chache baada ya taarifa rasmi kuwa Sammy Lee ameachia rasmi wadhifa wake wa kocha msaidizi.

Southgate anataka kuunda jopo lake mwenyewe na anaona Lampard kama mtu atakayemfaa katika benchi lake.

Lampard ambaye alistaafu soka la kimataifa muda mfupi baada ya michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2014, ndio kwanza ameondoka New York City FC kufuatia kumaliza mkataba wake.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here