Na Mustafa Ismail
Waislamu
wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya sherehe za maulid ya kuadhimisha mazazi ya bwana mtume Muhammad
[s.a.w] ili kuonesha umoja na mapenzi kwa mtume
Akiongea na
waandishi wa habari jijini dar es salaam sheikh mkuu wa mkoa huo Alhadi
Musa Salum amewatakawaislamu kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo
yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja siku ya juma pili ya tarehe
11/3/1438 hijriya sawa na 11/12/2016 miladiya
“Ndugu
waandishi wa habari tumewaita kwa jambo moja kubwa waislamu duniani kote hivi
sasa wanatarajia kupokea mazazi au kuzaliwa kwa kiongozi wao mtume Muhammad
[S.A.W]lakini pia kubwa tunalotaka kulizungumzia ni sherehe hizo kimkoa
zitafanyika katika viwanja vya mnazi mmoja siku ya jumapili ya tarehe
11/12/2016 kuanzia saa mbili usiku.”
Sheikh
Alhadi alisema kuwa mauled itasindikizwa na maandamano yatakayoa anza katika viwanza vya mnazi mmoja
na kupita katika barabara kadhaa jijini humo “ lakini pia shughli hiyo
itaandamana na maandamano yatakayoanza alasiri katika viwanja vya mnazi mmoja
kupitia morogoro road yatapitia katika barabara ya msimbazi yatatokea barabara
ya uhuru na kutokea katika barabara ya Lumumba na kurudi tena katika viwanja
vya mnazi mmoja.”
Aidha Sheikh
Alhadi aliwaomba waislamu wa mkoa wa Dar es salaam kusherehekea sikukuu hiyo
kwa amanai na utulivu na kwa namna itakayomridhisha mola wao huku akiwataka kujiepusha na uvunjaji wa
sheria na kuwataka kulinda umoja amani na mshikamano.
Mgeni rasmi
katika shere hiyo atakuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhajj Ali Hassan
Mwinyi ambaye ataongozana na viongozi wa vyama mbalimbali naviongozi wa kidini.
Kauli mbiu
ya mwaka huu ni muislamu jitambue badilika aamani ndio maisha yetu.
No comments:
Post a Comment