Mbunge mmoja nchini Uingereza
amesema kuwa mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anafaa
kuchunguzwa na maafisa wa Uingereza kufuatia madai kwamba alitumia
kampuni za kigeni kupunguza kodi anayolipa.
Hatahivyo ajenti wa mkufunzi huo amesema kuwa madai hayo hayana msingi wowote.
Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mali ya umma Meg Hillier aliambia Gazeti la Sunday Times kwamba madai hayo yanafaa kuchunguzwa.
Shirika la mapato na kodi nchini humo limesema kuwa halitatoa tamko lolote kuhusu watu waliotajwa ,lakini linachukulia madai yote ya kukwepa kulipa kodi na umuhimu mkubwa na kwamba litachunguza madai ya udanganyifu pamoja ushahidi unaotolewa.
No comments:
Post a Comment