KAMA UNAAMINI KUWA MAMA NI MAMA NA DUNIANI TUNAPITA BASI SOMA HABARI HII - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Sunday, December 4

KAMA UNAAMINI KUWA MAMA NI MAMA NA DUNIANI TUNAPITA BASI SOMA HABARI HII

                                Image result for DUNIA
Napenda kukushirikisha habari hizi kwa kuwa muda ni kukumbushana na kama sote bina adamu ni vyema kuwaheshimu wazazi wetu hata kama pengine wamekwisha tangulia mbele za haki ni vizuri kuwakumbuka jkwa mema pia.

nakupa mfano kwa  story hii kidogo usome na kisha kuelewa kwa umakini
Penseli: "Nisamehe sana"
Ufutio: kwa nini? Mbona hujanikosea lolote?
Penseli: Nisamehe sana unaumia kwa ajili yangu, kila ninapofanya makosa siku zote upo kwa ajili ya kuyafuta, ila kila unapofuta makosa yangu unaumia na kupoteza sehemu yako na umaendelea kupungua kadiri unavyofuta makosa yangu.
Ufutio: Ni kweli, ila mimi sijali sana. Hiyo ni kazi yangu, niliumbwa kwa ajili ya kukusaidia kila pale utakapokosea ingawa najua siku moja nitaisha na kupotea kabisa, ila nina furaha na kazi ninayoifanya. Hivyo usijali najisikia vibaya ukiwa na huzuni.
Penseli: Nashukuru sana ufutio.
_____________________________________
Wazazi wetu ni kama ufutio, na sisi watoto zao ni kama penseli. Siku zote wazazi wetu wapo kwa ajili yetu kufuta makosa yetu na kutuelekeza njia zipaswazo kupita, na wafanyapo haya muda mwingine huumia hudharauliwa na kutengwa lakini wamesimama kidete kuhakikisha tunastawi vema.
Watunze sana wazazi wako (kama wapo na wale ambao wameshatangulia mbele ya haki Mwenyezi Mungu awerehemu) waheshimu na kuwapenda siku zote.
Mwenyezi Mungu awape wazazi wako maisha marefu yaliyojaa heri, fanaka na afya tele!
Kwanini tusiseme AMEN!
Share kwa wengine habari hii

1 comment:

Post Top Ad

Responsive Ads Here