KOCHA WA ARSENAL,ARSENE WENGER ATOA TAMKO JUU YA SANCHEZ NA OZIL - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, December 8

KOCHA WA ARSENAL,ARSENE WENGER ATOA TAMKO JUU YA SANCHEZ NA OZIL

Image result for wenger
Arsene Wenger amesema Arsenal haitawauza Alexis Sanchez na Mesut Ozil hata kama hawatasaini Mikataba Mipya.

Masta hao wakubwa ambao ni tegemezi kubwa kwa Arsenal wamebakiza Miezi 18 katika Mikataba yao ya sasa lakini mpaka sasa hawajaafiki kusaini Mikataba Mipya ya Nyongeza.

Sanchez na Ozil wanataka Nyongeza kubwa ya Mishahara yao ili wavune kama Mastaa wengine wakubwa lakini Menejimenti ya Arsenal imekataa hilo.
Wawili hao, Msimu huu wameifungia Arsenal Jumla ya Mabao 21.

Akiongelea hali ya sasa, Wenger ameeleza: “Hata iweje watabaki kwa Miezi 18 iliyobaki na labda zaidi ya hapo.”
Aliongeza: “Wachezaji hawa watabaki si chini ya Miezi 18 lakinimmazungumzo yanaendelea lakini si ya kuwekwa wazi.’

Ingawa Wenger ana matumaini makubakia kwa Ozil na Sanchez lakini ameshindwa kuwapa uhakika wowote Mashabiki wa Arsenal.

Alipohojiwa kama anawapa uhakika Mashabiki kuhusu kubakia kwa Wawili hao, Wenger alijibu: “Hapana. Wana Miezi 18 ya Mikataba yao na wataendelea kucheza wakiwa hapa. Baada ya hapo itabidi Mikataba iongezwe lakini siwezi kuzungumzia suala katika kila Mahojiano na Wanahabari. Ni kawaida mkiongeza Mkataba kuna majadiliano.”

Hivi Sanchez anahusishwa na kuhamia huko Mashariki ya Mbali, hasa China, ambako imeripotiwa amepewa Ofay a ajabu ya kulipwa Pauni Laki 4 kwa Wiki.
Wenger amepasua: “Naamini hilo. 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here