TATHMINI YA ZORYA LUHANSK V MANCHESTER UNITED, MECHI YA MWISHO KUNDI A EUROPA LIGI,HII HAPA - MKWELITZ BLOG

Breaking

.

.

.

.

Thursday, December 8

TATHMINI YA ZORYA LUHANSK V MANCHESTER UNITED, MECHI YA MWISHO KUNDI A EUROPA LIGI,HII HAPA

Image result for manchester united
Alhamisi Usiku huko Nchini Ukraine, Manchester United wako Ugenini kucheza Mechi yao ya mwisho ya Kundi A la UEFA EUROPA LIGI wakihitaji Sare tu dhidi ya Zorya Luhansk ili kufuzu Raundi ya Mtoano ya Timu 32.
Zorya Luhansk tayari wapo nje ya Mashindano.
Mechi nyingine ya Kundi A ni kati ya Feyenoord na Fenerbahce huko Rotterdam na Fenerbahce wanahitaji Sare tu ili kusonga.
Mechi ya Zorya na Man United haichezwi Nyumbani kwa Timu hiyo Mji wa Luhansk na badala yake ipo Mji wa Odessa kutokana na machafuko ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Ingawa Man United wanahitaji sare tu ili kuvuka lakini wanaweza hata kufungwa na kufuzu ikiwa tu Feyenoord hawashindi.
Ili kumaliza Nafasi ya Kwanza ya Kundi, Man United wanahitaji kupata Matokeo bora kupita Fenerbahce.
Umuhimu wa Timu kumaliza Nafasi ya Kwanza ya Kundi unakuja kwenye Droo ya Raundi ya Mtoano ambapo Washindi wa Makundi hawapangwi na Washindi wengine wa Kundi na pia hawakutanishwi na Timu za juu kwa Ubora kutoka zile Timu 8 zinazotupwa EUROPA LIGI kutoka UEFA CHAMPIONZ LIGI zilizomaliza Nafasi za 3 za Makundi yao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here