Ben Pol
Ben Pol amesema maombi hayo ya mrembo ‘Ebitoke’ aliyaona mitandaoni tangia jana ila hakuamini kwani alijua ni stori tuu za mitandaoni mpaka leo baada ya kuona video ikisambaa Instagram ikimuonesha mrembo huyo akibubujikwa na machozi huku akimtaka amuoe.
“Kweli nimeziona habari mitandaoni tuu tangia jana watu wakiposti lakini sikuamini siunajua habari za mitandao bro! ila leo pia nimeona video yake akisisitiza ombi lake lakini bado siamini na nitaamini na nitafurahi kama tukionana uso kwa uso.”amesema Ben Pol kwenye mahojiano yake na Bongo5.
Hata hivyo Ben Pol amesema anaheshimu sana hisia za kila mtu na kitendo cha Ebitoke kutamka hadharani kuwa anavutiwa nae amekiheshimu na kukichukulia kwa uzito.
“Kwanza niseme tuu naheshimu hisia za kila mtu yeye ni binadamu na ameonesha hisia zake soo naziheshimu sana.“amesema Ben Pol.
Ben Pol ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Tatu’ aliyomshirikisha Darassa, wiki tatu zilizopita alikuwa ni gumzo mitandaoni baada ya kuposti picha iliyoleta utata mitandaoni.
No comments:
Post a Comment